Tuesday 10 May 2011

Wema Sepetu apandishwa kizimbani

Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu, amepanda kizimbani kujibu shitaka la kumtukana matusi ya nguoni Raheem Rummy "Rais wa Masharobaro".
Wema (26), ambaye pia ni nyota wa filamu nchini, alipandishwa kizimbani jana asubuhi katika Mahakama ya Mwanzo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mfawidhi Mariam Masamalo.
Mrembo huyo alifikishwa mahakamani hapo akiwa na baadhi ya wasanii wenzake wa filamu akiwemo Rose Ndauka, ambaye alikuwepo mahakamani hapo hadi saa 7:00 mchana kesi hiyo iliposomwa.
Akisoma shitaka hilo, Karani Sharifa Dunia, alidai kuwa, Aprili 11, mwaka huu, saa 12.38 jioni huko Kinondoni alimtukana Rummy.
Hakimu Mariam alimuuliza Wema sababu za kutukana matusi hayo na mrembo huyo alisema ilikuwa ni hasira tu.
Baada ya baadhi ya waandishi kutoka nje, waliwashuhudia Rose Ndauka na mtu aliyedaiwa kuwa ni mama mzazi wa Wema wakijadiliana juu ya dhamana ya mshitakiwa huyo. Aliachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili waliotia saini ya ahadi ya Sh. 300,000.
Kesi imepangwa kuja tena mahakamani hapo Mei 18, mwaka huu.
Wema nara kwa mara amekuwa na matatizo ya katika vyombo vya sheria na wakati fulani aliwahi kulala rumande kwa siku kadhaa katika kesi ya tuhuma za kuvunja kioo cha gari la aliyedaiwa kuwa 'boifrendi' wake wa zamani, muigizaji Steven Kanumba.

No comments: