Tuesday, 10 May 2011

KCU chawaongeza malipo wakulima wa kahawa

Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kagera (KCU), kimepitisha malipo ya nyongeza kwa wakulima wa kahawa waliokiuzia chama hicho kahawa kwa msimu wa mwaka 2009/2010.
Meneja Mkuu wa Chama hicho, Vedasto Ngaiza aliyasema hayo wakati wa mkutano mkuu wa mizania wa KCU wa kujadili ununuzi wa kahawa wa msimu mwaka 2009/10 uliofanyika wiki iliyopita katika ukumbi wa hoteli ya Bukop inayoimiliki.
Ngaiza, alisema wajibu wa mkutano huo ni kuhakikisha wakulima wa zao la kahawa waliokiuzia chama hicho kahawa ya maganda aina ya Robusta wanalipwa fedha ya ziada ya Sh. 44 kwa kila kilo
Alisema wakulima walikiuzia chama hicho kahawa ya maganda aina ya Arabica wataongezewa Sh. 32 kwa kila moja
Alisema fedha za ziada itakayotolewa kwa wakulima ni sehemu ya faida ambayo chama hicho kimeipata katika msimu wa ununuzi wa kahawa wa mwaka 2009/2010.
Alisema kuwa soko la kahawa katika msimu huo lilikuwa zuri kidogo
ikilinganishwa na msimu wa ununuzi wa kahawa wa mwaka 2008/2009.
Ngaiza alisema katika msimu wa ununuzi wa kahawa wa mwaka 2008/2009 kilifanya mauzo ya kahawa kwenye soko yenye thamani ya Sh. Bilioni 1.06 katika msimu huo na kwamba kilikuwa kimeweka lengo la kukusanya Sh. Bilioni 1.3 katika mauzo yake kwenye msimu huo.

No comments: