Friday 6 May 2011

RAIS JAKAYA AWAAPISHA MANAIBU KATIBU WAKUU IKULU DAR JANA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha John Thomas Mngodo kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Anna Maembe kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Sihaba Nkinga kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Charles Amos kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Alphayo Kidata Ikulu (nafasi moja) wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Hab Mkwizu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma wakati wa hafla fupi ya kuapishwa Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Jakaya Kikwete Makamu wake Dkt Mohamed Gharib Bilal wakipiga picha ya kumbukumbi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Eng. Mussa Ibrahim akiwa na familia yake baada ya kuapishwa rasmi jana.
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Waziri wa Ujenzi Mh. John Pombe Maghufuli, wakati wa hafla ya kuwaapisha Manaibu Katibu Wakuu Ikulu Dar es Salaam jana..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia na mtoto Irene Simba ambaye ni mtoto wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Juma Malemi (kushoto) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Manaibu Katibu Wakuu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Familia ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Juma Malemi baada ya kuapishwa rasmi kwenye hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam jana. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Familia ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Anna Maembe baada ya kuapishwa rasmi leo kwenye hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam.

Al-Qaeda yathibitisha kifo cha Osama

Al-Qaeda imethibitisha kifo cha kiongozi wake, Osama Bin aden, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi hilo na kutangazwa kupitia mitandao mbalimbali ya itikadi kali.
Taarifa
Taarifa inayothibitisha kifo
Tarifa hiyo imesema damu ya kiongozi huyo "haitapotea" na kuwa al-Qaeda itaendelea kushambulia Marekani na washirika wake.
Kifo cha Bin Laden kitakuwa "laana" kwa Marekani, na kutoa wito kwa Pakistan kuanza harakani, imesema taarifa hiyo.
Bin Laden alipigwa risasi na kufa siku ya Jumatatu, wakati makomando wa Marekani walipovamia nyumba yake katika mji wa Abbottabad nchini Pakistan.
Osama
Osama Bin Laden
Uvamizi huo ulifanywa bila ya mamlka za Pakistan kufahamu, na hivyo kuongeza mvutano kati ya nchi hizo mbili.
Mikutano kadhaa ya hadhara inafanyika nchini Pakistan siku ya Ijumaa, kupinga hatua hiyo.
Taarifa hiyo iliyochapishwa katika mitandao yenye itikadi kali imesema sauti ya kiongozi huyo wa al-Qaeda iliyorekodiwa wiki moja kabla ya kifo chake itatolewa hivi karibuni.
Nyumba
Makazi ya Bin Laden, Pakistan
"Damu ya Osama Bin Laden itaendelea kubaki, kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, laana inayowafuata wamarekani na jamaa zao, itawafuata ndani na nje ya nchi zao," imeonya taarifa hiyo.
"Furaha yao itakuwa masikitiko, na damu yao itachanganyika na machozi. Tunatoa wito kwa Waisilamu wenzetu nchini Pakistan, ambao katika ardhi yao Sheikh Osama aliuawa, wasimame na kupambana."
Waandishi wa habari wanasema Wapakistani wengi wamekasirishwa na kile wanachoona kama Marekani kuingilia uhuru wa nchi yao.
US
Marekani wakisherekea kifo cha Osama
Pia wanaishutumu serikali ya Pakistan kwa kuruhusu makomando wa Marekani kufanya shughuli zao, ingawa maafisa wanakanusha kuwa walifahamishwa.
Karibu watu 1,000 walikusanyika katikati ya mji wa Abbotabad baada ya sala ya Ijumaa, limeripoti shirika la habari la AFP.
Walichoma moto matairi ya magari, kuweka vikwazo katika barabara kuu na kupiga kelele wakisema "Hapana Marekani" na "magaisi, magaidi, Marekani ni magaidi".
Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Rawalpindi amesema maandamano ya kupinga Marekani yalikuwa madogo kuliko yalivyotarajiwa, huku watu 50 wakijitokeza.

Fainali ya wanavitimbi,Je ni nani atajinyakulia ushindi kati ya hawa?

Lile shindano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa vichekesho Bongo, linatarajiwa kufanyika kesho ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, Dar es Salaam ambapo patakuwa hapatoshi.

Akizungumza na Ijumaa, mratibu wa shindano hilo, Imelda Mtema alisema kuwa,  mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan na kiingilio kitakuwa shilingi 8,000.

Aidha, mratibu huyo alisema kuwa, washiriki wote wa shindano hilo lililoendeshwa na Gazeti la Risasi kwa muda wa miezi minne, wamejiandaa vizuri.

Alizitaja zawadi za washindi kuwa, mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Tsh.1,500,000, wa pili 1,000,000 na 500,000 kwa mshindi wa tatu.

Washiriki watakaoshika nafasi ya nne na tano, watapata kifuta jasho cha Tsh. 250,000.
Shindano hilo litapambwa na burudani kutoka Bendi ya muziki wa dansi nchini,  African Stars International ’Twanga Pepeta’ na wasanii wa miondoko ya kizazi kipya, Sam Morgan, TMK Unit, Tox Star na Ziro 4.

Shindano hilo limedhaminiwa na Allure International Model, Dar es Salaam City College- Kimara, Jarida la Malaika, Cream Pub- Kinondoni, Dotnata Decoration, Manywele Beauty Cosmetics na ASET Ltd.

Washiriki waliotajwa kuwania tuzo hizo ni Joti, King Majuto, Masanja Mkandamizaji, Kingwendu (pichani) na Masele.

Kama unawafagilia, endelea kupiga kura, unaweza ukamsaidia yule unayetaka aibuke mshindi.
Jinsi ya kupiga kura, andika jina la mshiriki unayependa ashinde katika sehemu ya ujumbe wa simu kisha tuma kwenda 0788 240 136

Tanzania: Nation Wins Credit On Capital Controls

TANZANIA is one of the countries in Sub-Saharan Africa with tight capital controls that discourage speculative inflows.


According to the International Monetary Fund (IMF) Regional Economic Outlook report Sub-Saharan Africa, released on Tuesday indicates that the move was aimed at coping with external shocks and especially after the world financial crisis experience.
The report says that high levels of foreign inflows into relatively small economies had posed challenges for policy in several countries.
"The high levels of capital flow into emerging economies before the crisis posed several challenges but again when investors pulled out, it led to increased exchange rate instability," the report says.
It says some countries may consider temporary controls on capital inflows to try to mitigate a recurrence of such instability. "The long-term trend has been toward more open capital accounts," the report says.
Commenting on the report, Dr Honest Ngowi, a senior lecturer with Mzumbe University Dar es Salaam Campus says that cautious measures should be adopted before liberalizing capital account.
"Generally it is risky and should not be left to be controlled by market forces. But if done with diligence, the country might reap enormous benefits from investment flows," he says.
He says the central bank should consider all possible effects and implications of liberalizing its capital account to the national economy.
The IMF report reveals further that private capital inflows had not yet returned to pre-crisis levels in all areas. "Private investors, possibly still smarting from the global financial losses of recent years, seem to be distinguishing between markets," the report says.
However, the economic growth in sub-Saharan Africa has largely returned to pre-financial crisis levels despite its monetary tightening failing to keep pace, with rising fuel and food prices a growing threat.
The IMF reiterated its forecast of 5.5 per cent Gross Domestic Product (GDP) growth for the region this year and 5.9 per cent in 2012, with low-income countries that make up the bulk of the continent recovering the fastest.
But the report warns over the rising food and fuel prices which tested the region's resilience of the past few years once again.
"These price shocks, coupled with the recovery, are likely to lead to higher inflation in most countries and to deteriorating current account deficits in a number of fuel importers," it says, adding:
"Monetary policy remains looser than desirable in many countries at the region ... Interest rates have failed to keep pace with the cyclical recovery and policy now needs to move ahead of the curve," it said.

Dk. Shein ukiwasahau vijana ‘watakupotezea’


USEMI huu uliwahi kuandikwa katika baadhi ya vitabu vingi vya mwandishi gwiji Afrika Mashariki na pengine Kusini mwa Jangwa la Sahara marehemu Shaaban Robert au ufukwe ambao ni maarufu sana usemao watoto wa leo ni taifa la kesho.
Utoto unaelezwa ni ule wa rika kati ya siku moja hadi miaka 15,baada ya hapo mtoto hubadilika jina na kuitwa kijana, ujana ni kuanzia kati ya miaka 18- 45, hili ndilo hasa rika kamili la ujana kadri nijuvyo.
Kwa mujibu wa Shaaban Robert kijana ni Taifa la leo.
Taifa la leo kwa mantiki ya kuwa nguvu kazi na tegemezi kuu katika wakati uliopo ili ajenge nchi na kutumika ipasavyo katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Ukweli unaoonyesha kuwa vijana katika Afrika na hasa Visiwani Zanzibar ni mithili ya tingatinga au greda linaloweza kufumua vifusi, miamba, milima na hatimaye kunyoosha njia iliyokuwa na tabu ya mashimo, mabonde na makorongo makubwa kisha waruhusiwe wazee kupita na kujinafasi buheri hamsa wa ishirini.
Katika nchi nyingi za kiafrika Vijana hutumiwa kama mihuri ya kuhalalishia tawala za wazee.
Jambo hilo pengine ndilo linalowafanya wazee hao baada ya kuzeeka laana ya kulichukia rika la ujana huwangukia na kuanza kupigwa vigongo vya utosi. Hapana nieleweke sihimizi mauaji ya vikongwe.
Nimejikuta nikilazimika kuyaandika makala haya huku nikiawa na kumbukumbu nyingi ndani ya kichwani changu kabla na baada ya Mapinduzi ya 1964 Visiwani Zanzibar.Kila nikilitazama kundi au rika la Vijana lilivyotumikishwa na linavyotumikishwa, nashindwa kuwatofautisha wao na matumizi ya kondomu kwa binadamu.
Ni mja gani huyo mjinga anayeweza kuithamini kondom ikiwa hana haja nayo kwa wakati maalumu mahali fulani na kwasababu husika? Hata kuibeba huwa ni aibu na fedheha isiyomithilika.
Katika historia ya kweli vijana ndiyo walioamsha vuguvugu la kutaka mabadiliko ya haraka baada ya kuchoshwa na ukandamiziaji uliokuwa ukifanywa na wageni waliokuwa wakiwabagua waafrika walio wengi na kuwanyima baadhi ya fursa muhimu.
Umoja wa vijana wa chama cha ASP, ASP Youth League hapa Zanzibar ulikuwa mstari wa mbele kushajihisha hamasa za kisiasa baina ya mashamba na maeneo ya mijini huko Pemba na Unguja na kuweka mikakati ya kuudondosha utawala wa kisultan madarakani.
Siku ya Mapinduzi, vijana ndio waliokuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nchi inabaki mikononi mwa wazalendo, lakini cha kushangaza kundi la wazee likajitokeza na kujihesabu kuwa wao ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika Mapinduzi.
Hata Mzee Abeid Karume alikiri kwamba hakuwamo katika kundi la watu wanaoitwa ‘Member of 14’ wakati Mapinduzi yakifanyika na kwamba siku alikuwa amejificha Dar es Salaam kwa sababu za kiusalama.
Ni jambo la kweli wazee wa ASP kwamba walishiriki kupanga na kufanya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 lakini ikumbukwe pia na iaminike kuwa walioshiriki kikamilifu katika mapambano ya ana kwa ana na ya kufa na kupona ni kundi kubwa la vijana.
Baada ya Mapinduzi kufanikiwa wazee karibu wote ndiyo walioshika madaraka ya juu katika SMZ ikiwamo wao kuwa MBM, mawaziri, wakuu wa mikoa, makatibu wakuu na makamishna. Vijana wakajikuta wakitiwa mchanga wa macho.
Hata hivyo, sehemu kubwa ya wanasiasa vijana waliokuwa hodari na wasomi walipotea katika mazingira ya utatanishi ulioambatana na chuki na hadi leo hii hawajulikani kama wako hai,wamezeeka sana au wako katika gereza fulani hapa Zanzibar au huko Tanganyika.
Inaaminika kuwa kupotea na kuyayuka kwao kulitokana na hofu iliyowajaa wazee ili wasiwekwe pembeni katika kuiendesha nchi kutokana na wao kuwa na elimu kidogo na wengine kukosa miwani kabisa.
Kundi la vijana kwa mara ya kwanza lilipewa nafasi na Rais wa Awamu ya Pili, Zanzibar Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi alipoamua bila ya hofu kuwapa vyeo na kuwaingiza serikalini baadhi ya vijana hodari wakiwamo Seif Sharif Hamad, Salmin Amour Juma, Khatib Hassan Khatib, Soud Yussuf Mgeni na Omar Ramadhan Mapuri.
Kundi hili la mrengo wa kushoto kwa sehemu kubwa lilithbutu kunyoosha vidole vyao juu na kuhitaji yafanyike mabadiliko zaidi wakati huo likijiita ‘Progressive Team’ huku likichuana kwa nguvu ya hoja na lile la wazee lililokuwa likiitwa Liberators Mob.
Wazee walikuwa ni kina Abdallah Natepe, Hassan Nassor Moyo, Jamal Ramadhan Nassib, Ramadhan Haji Faki, Khamis Daruwesh na wengine.
Kundi la vijana lililokuja kuwa imara kabla ya kugawanywa kwa fitna na vitisho lilikuwa la kina Ali Ameir Mohamed, Shaaban Khamis Mloo, Ali Haji Pandu, Isaac Sepetu, Adam Mwakanjuki, Salmin Amour na wengine.
Wazee kwa kiasi kikubwa na mara zote waliwatuhumu na kuwabatiza Vijana hao majina mabaya na kudai kwamba ni kundi la wasaliti na mamluki wapya wanaotaka kuyatosa na kuyapoteza Mapinduzi ili kuurejesha usultan visiwani Zanzibar.
Awamu ya tatu ilipofika, kidogo chini ya Rais Ali Hasssan Mwinyi kwa kipindi kifupi ilikuja na mkakati wa kuzibeba sura mpya katika kundi la vijana hao na kufanikiwa lakini awamu ya tano, sita na saba hofu ya vijana ikawapata tena watawala wetu.
Dk. Shein ameanza kulitosa kundi la vijana, lakini na yeye asishangae wala kustaajabu ikiwa nao wataamua na kujipanga ili kumpotezea mwaka 2015.
Sijajua ni kwa sababu gani hasa inayowasibu na kuwajaza woga usiokadirika viongozi wazee kuwatenga vijana, pengine ninachoweza kusema ni kuhofia ujio wa mabadiliko kwa mwendo wa haraka na kuwashangaza wazee hao ambao baadhi yao sasa wanajikongoja wakipungukiwa nguvu, maarifa na kusimamia maamuzi magumu.
Matumaini makubwa ya vijana yalikuwa ni kwa Rais mpya Dk. Ali Mohamed Shein.
Matumaini na matarajio hayo sasa yamezamishwa katika mkondo mkali wa Nungwi na hayaonekani kuwapa nafuu tena kwa upande wa vijana.
Uteuzi wake ulioanzia katika nafasi za kisiasa na kitaaluma bada ya kuukwa urais anaonekana kuwababeba wazee wenziwe na kuwatosa vijana ambao aliwatumia bila kuchoka katika hamsa za kumfanyia kampeni hadi kupata ushindi uliomweka Ikulu.
Vijana wa leo si wale wa baada ya Mapinduzi ya Zanzibar 1964, ni wasomi, wepesi, wachapakazi na wajuzi katika fani mbalimbali, Rais Dk. Shein amefuumba macho yake na kuteua wastaafu kama kwamba hakuna vijana wapywa na wataalamu
Nimneona nimtumie salamu za haraka Dk. Shein na kumtaka atanabahai ili kufuata nyayo za Rais Jakaya Kikwete wa Tanganyika ambaye amekubali kuteua na kuwapa nafasi nyeti katika Serikali yake sehemu kubwa ya kundi la vijana.
Katika Ofisi za Serikali huko Tanganyika leo hii kuanzia kwenye halmashauri za wilaya, manispaa, ofisi za wakuu wa wilaya na mikoa na kwenye wizara za Serikali Kuu kumetamalaki vijana wasomi ingawaje na baadhi ya wazee wapo wakiwashindikiza vijana wao.
Ni kinyume kabisa cha mambo yalivyo hapa Zanzibar. Vijana wametiwa chachu na huachwa wapige maneno mabarazani, wamezoea kulambishwa pipi huku baadhi yao wakijilia urojo na wengine wakiamua kubwia unga na kujiajiri katika ajira hatarishi.
Dk. Shein akumbuke na ajaribu kuvuta picha ya wakati wa kampeni zake akiwa Pemba na Unguja, ni kina nani hasa waliokuwa wakijaza kwenye magari na kupeperusha bendera ya chama kilichompa ushindi, ni wazee au vijana?
Kitendo chake cha kuendelea kuzifanya ajira za Serikali kama zenye hatimiliki kwa kundi moja la watu wenye itikadi ile ile anayoitii yeye ni kwenda kinyume cha ukweli wa mambo ulivyo,hii ni hatari nyeusi katika siku zijazo.
Vijana ni vijana wako wengi na wanahitaji kuangaliwa na kusikilizwa. Wakifumbwa midomo iko siku wataifumbua na hawataiziba ng’o.
Vijana wa Zanzibar ni wavumilivu sana, wastaarabu, wenye heshima, wengi kati yao wameamua kusafiri na kuishi ughaibuni, hawakutaka kuitegemea Serikali yao hivyo ni vema kwa hawa wachache waliopo wakasaidiwa na kupewa vijikazi.
Wakiendelea kubaki vijiweni na mabarazani toka asubuhi hadi jioni wanaweza kupotoka, wanaweza kuamua kufanya uasharati,umalaya na kucheza kiduku huku wazee wao wakitanua kwa kukaangiza pilau ya michele ya basmati huku vijana wakila wali uliopikwa kwa mchele wa mapembe na kitoweo cha dagaa la kuosha.
Nafasi pekee ambayo nilifikiri Rais Dk. Shein ingeliweza kumpatia umaarufu na kujijengea matumaini ya matumaini ya kuungwa mkono zaidi ni kuligusa kundi hili, kulipa imani kundi la vijana na kuwaajiri katika nafasi za juu serikalini.
Angefanya hayo, angehesabiwa amelamba turufu na kujenga mtaji usio na shaka ifikapo mwaka 2015 kama angeamua sasa kuteua vijana wapya na kuwapa nafasi serikalini.
Ninamheshimu sana Dk. Shein, ni mtu makini, anyefuata taratibu, si mtu anayetegemea siasa za udaku na umbea. Anathamini Umoja wa Kitaifa lakini kwa kuliweka pembeni kundi la vijana naona kama anatamani asitoke mrisi katika mchezo wa karata katika uchaguzi ujao.

Watoto wa aliyekuwa Mfalme wa Mziki wa Pop Michael Jackson watoa msaada kwa waathirika wa Sunami Japan

WATOTO wa aliyekuwa mfalme wa pop, Michael Jackson, wameguswa na janga lililoikumba Japan hivi karibuni na kuamua kuchangia nguo za kuwapa walioponyeka kwenye maafa hayo.
Shangazi wa watoto hao, La Toya Jackson, alibainisha watoto hao, Prince Michael, Paris na Blanket wameguswa moja kwa moja na tukio hilo na hivyo kuamua kutoa walichonacho kwa watoto wenzao.
Michango mbalimbali ya misaada imekuwa ikihamasishwa kutolewa kwa ajili ya kuwasaidia walioathirika na janga la tetemeko la tsunami na watoto hao wa nyota wa muziki wa pop duniani, Michael Jackson wamebainisha kuwa na kitu kidogo cha kuchangia.


La Toya aliiambia OKmagazine.com, “Hawakujali wanafanya nini au wanatoa kitu gani. Ilikuwa safi sana. Walisema, ‘Tunaweza kuwapa nguo zetu?’ Ilikuwa safi sana.”
La Toya alisema kwamba familia ya Jackson imefarijika kwa kuwapeleka watoto hao wa mwimbaji wa “Thriller” katika matukio kama hayo ya michango ya kihisani.

Osama’ mpya aamuru Uingereza ‘ifundishwe adabu


Rais Obama Marekani ametofautiana na Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) kuhusu kuchapishwa hadharani kwa picha za mwili wa Kiongozi wa Kikundi cha Ugaidi cha Al Qaeda, Osama bin Laden.
Wakati Mkurugenzi huyo, Leon Panetta akisema picha hizo zitatolewa hadharani kuzima ubishi unaoendelea iwapo kweli mwasisi na kiongozi huyo wa al-Qaeda ameuawa na makomando wa Marekani nchini Pakistan usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii, bosi wake amepingana naye.
Jumapili, Panetta, ambaye aliteuliwa hivi karibuni na Rais Obama kuwa Waziri wa Ulinzi, aligeuka shujaa machoni mwa wengi kwa kuisimamia vyema operesheni hiyo.
Kufikia juzi, Obama alimpinga, akisema hakuna haja ya kutoa picha za kutisha za mwili huku akiungwa mkono na mawaziri wake wawili akiwamo Waziri wa Ulinzi anayeondoka, Robert Gates na Waziri wa Mambo ya Nje, Hillary Clinton.
Akitangaza uamuzi huo, Obama alisema: ‘Hatuhitaji kushindana kama mpira wa miguu katika suala hili baada ya usiku wa kujivunia wa shambulio wiki hii.”
Rais Obama amesema picha za mwili wa Osama zina uwezekano mkubwa wa kuchochea chuki iwapo zitatolewa.
Maofisa wa Marekani wamekuwa wakijadili iwapo wachapishe picha hizo kukabiliana na nadharia kwamba nchi hiyo imedanganya.
Lakini Obama anaamini kuwa picha hizo huenda zikazua hisia kali akisema:“sisi hatutaki kuonyesha picha hizi kama kikombe cha kujivunia cha kumwonyesha kila mtu.”
Kutofautiana huko kunaonesha mgawanyiko uliopo miongoni mwa maofisa waandamizi wa utawala huo kuhusu kutoa au kutotoa hadharani picha hizo.
Hilo limekuja chini ya saa 72 baada ya kipindi kizuri cha urais wa Obama.
Tofauti hiyo iko hadi kwa Wamarekani ikiwa haihusiani na siasa kwa sababu baadhi ya wanachama wa Republican na Democrat wameunga mkono uamuzi wa rais wa kutotoa picha hizo wakati wanachama wengine wa vyama hivyo wamemkosoa vikali rais.
Wabunge kadhaa na wasaidizi wa Ikulu walieleza kushangazwa kuona tukio kubwa la kumuua gaidi hatari duniani linavuruga furaha na ushindi uliopatikana.
Kwa sasa utawala wa Rais Obama pia unahangaika kufuta ukungu wa shaka kutokana na mkanganyiko wa taarifa zake juu ya mauaji ya kiongozi huyo wa al-Qaida yaliyotokea Abbottabad, Pakistan.
Ikulu ya Marekani inasema kwamba kilichosababisha taarifa za mwanzo kuhusiana na kifo hicho zisiwe kamili ni kile inachokiita ‘ukungu wa vita’.
Kikiwanukuu maofisa wa Ikulu hiyo, kituo cha televisheni cha NBC kimesema watu wote wanne waliouawa, akiwemo Bin Laden mwenyewe, hawakuwa na silaha.
Taarifa hiyo ni tofauti na mbili za mwanzo, ambazo nazo pia zilitofautiana.
Ya kwanza ilikuwa ya Rais Obama mwenyewe akitangaza kifo cha Bina Laden, ambayo alisema kiongozi huyo wa al-Qaida alikufa kutokana na majibizano ya risasi kati yake na makomando wa Marekani.
Ya pili ilitoka kwa Msemaji wa Ikulu Marekani, Jan Carney ambaye alisema kuwa si Bin Laden aliyekuwa amejihami kwa silaha, bali ni wenzake.
Hata hivyo, picha zilizochapishwa na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) zinaonyesha maiti za wanaume watatu zikiwa kwenye madimbwi ya damu, lakini hakuna silaha inayoonekana karibu yao.
Licha ya hayo, Rais Obama amekataa katakata kuchapisha picha za mkasa mzima ulivyokwenda, akirejea msimamo wa Ikulu yake kuwa zitakuwa kichocheo zaidi wafuasi wa Bin Laden.
“Hakuna shaka kuwa tumemuua Osama bin Laden, Lakini ni muhimu kwetu kuhakikisha picha zinazoonyesha mtu aliyepigwa risasi kichwani, hazisambai na kuwa kichocheo cha vurugu na silaha ya kufanyia propaganda,” Rais Obama alikaririwa akisema juzi.
Mwanasheria Mkuu Marekani, Eric Holder, amesisitiza msimamo wa serikali kwamba kuuawa kwa Bin Laden hakukukiuka sheria yoyote ya kimataifa, kwa vile makomando wa Marekani walishambuliwa kwanza na ndipo nao wakalazimika kujihami.
Mwanzoni, mauaji ya Bin Laden yalianza kuijenga upya taswira ya Rais Obama kwa Wamarekani, ambao waliyapokea kwa vifijo na nderemo wakiamini kuwa kiongozi wao amesimamia kauli yake aliyoitoa tangu mwanzo.
“Nina furaha kwamba tuna rais ambaye amehakikisha jambo hili kalikamilisha. Na siyo rais ambaye amepoteza lengo, kama alivyokuwa George Bush, ambaye badala ya kumshughulikia Osama, akajielekeza Irak. Nafikiri hivi alivyofanya Obama ndivyo serikali makini inavyotakiwa iwe,” anasema Tyler, kijana wa miaka 30 anayeishi mjini Washington.
Matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa kwa ushirikiano wa Reuters na kampuni ya Ipsos na kuchapishwa Jumanne, yalionyesha kuwa mauaji ya Bin Laden yamepandisha imani ya Wamarekani kwa Rais Obama, ambaye anakabiliwa na uchaguzi hapo mwakani, wakiamini ameonyesha uongozi mzuri panapohusika suala la vita dhidi ya ugaidi.
Lakini kuanza kuibuka kwa taarifa mpya kila siku kuhusiana na namna mauaji yenyewe yalivyotokea, huku kila taarifa mpya ikipingana na nyingine na wasaidizi wa Ikulu wakitofautiana kuhusu utoaji picha, kumezua wasiwasi na kubadili maoni ya watu, si ndani ya Marekani tu, bali hata nje.
Wakati huohuo kiongozi mpya wa al-Qaeda ameelezea mpango wa mashambulio Uingereza katika barua pepe aliyomtumia mwandishi mmoja kachero wa gazeti la the Sun.
Anwar al-Awlaki anayeishi Yemen na ambaye anaaminiwa atakuwa badala ya Osama Bin Laden, ametaka mashambulio kama ya Mumbai, India, yafanywe Uingereza.
Majasusi wa Shirika la Ujasusi la Uingereza (M16) jana usiku walikuwa wakichunguza mawasiliano yake kwneye mtandao wa intaneti.
Katika barua yake pepe alisema: Tunachoweza kufanya ni kulipua mabomu katika maeneo mbalimbali, kufanya mauaji au kuyafyatulia risasi makundi ya adui.”
Pendekezo la mwisho linaelekea kuonyesha mashambulio ya mabomi yaliyotokea Mumbai, India ambako watu 164 waliuawa mwaka 2008.
Awlaki (40), amekwisha kuongoza majaribio ya mashambulio Uingereza na Marekani.
Alimshawishi mwanafunzi mwenye umri wa miaka 21, Roshonara Choudhry kumchoma kisu Mbunge wa Chama cha Labour, Stephen Timms kwa kuunga mkono uvamizi wa Marekani na Uingereza nchini Irak.

mke wa waziri wa masuala ya kijasusi, amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Bi Sheryl Cwele
Cwele, aliyeolewa na Siyabonga Cwele, alikuwa akiajiri wanawake kuingiza dawa hizo nchini Afrika kusini kutoka Uturuki na Marekani ya kusini.
Cwele alikutwa na hatia pamoja na mwenzake Frank Nabolisa, raia wa Nigera, katika mahakama kuu ya Pietermaritzburg.
Mshirika wake huyo Nabolisa naye amepewa hukumu hiyo hiyo ya miaka 12.
Madai ya biashara ya dawa za kulevya yalianza mwaka 2009 baada ya kukamatwa kwa mwanamke mmoja raia wa Afrika kusini aliyekamatwa Brazil na aina ya cocaine yenye thamani ya dola za kimarekani 300,000.
Tessa Beetge kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka nane gerezani mjini Sao Paulo.
Alikutwa na kilo 10 za coaccaine kwenye mkoba wake.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji Piet Koen alielezea makosa yao kuwa mazito mno.
Alisema, " Familia nyingi zinaathiriwa na dawa za kulevya zinazoletwa hapa kinyume cha sheria. Huteseka kutokana na wafanyabiashara wanaosababisha kutawaliwa na usambazaji wa mara kwa mara na kujikuta wakiwa wanaendela kutumia dawa hizo.
Watu hao wawili, ambao walikana mashtaka, walisema watakata rufaa dhidi ya hatia yao ya kufanya biashara hiyo.
Wangeweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.
Upinzani umetoa wito wa kumtaka Bw Cwele ajiuzulu, ukisema kama hajui shughuli za mkewe zilizo kinyume cha sheria, basi hana haja ya kuendelea kuongoza kitengo cha kijasusi nchini humo.

Besigye kupelekwa ng'ambo kwa matibabu

Dr. Kizza Besigye
Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye atapelekwa ng'ambo kwa matibabu zaidi.
Mkewe kiongozi huyo Bi Winnie Byanyima aliambia BBC kuwa madaktari wanaomshughulikia mwanasiasa huo katika hospitali moja Mjini Nairobi wanahofia kuwa Besigye alipata madhara makubwa ya sumu kwenye ngozi na macho yake.
Kiongozi huyo wa upinzani alisafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya kupigwa na polisi wa Uganda wakati wa kuzima maandamano aliyokuwa akiongoza ya kutembea kwa miguu hadi kazini kupinga kuongezeka kwa gharama ya maisha nchini Uganda.
Bi Byanyima amemuomba Rais Yoweri Museveni kufanya mashauriano na upinzani pamoja na viongozi wa Kidini ili kutafuta suluhu juu ya matatizo yanayoikumba Uganda badala ya kuwa timua nguvu kupita kiasi kutawanya maandamano.

Obama azuru eneo la mashambulizi 9/11

Rais Obama
Rais Obama akiweka shada la maua katika eneo la mashambulizi mjini New York.
Rais wa Marekani Barack Obama amezuru eneo ambalo mashambulizi ya 11 Septemba yalitokea mjini New York.
Ziara hiyo inafanyika siku nne baada ya kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Al-Qaeda Osama Bin Laden, nchini Pakistan.
Inaaminika Bin Laden ndiye aliyepanga mashambulizi hayo ya 9/11 mwaka wa 2001.
Rais Obama aliweka shada la maua kuwakumbuka takriban watu 3000 waliofariki na pia kuzungumza na jamaa zao katika eneo hilo.
Awali Obama aliwaambia maafisa wa kikosi cha kuzima moto kuwa: ''Wakati tunaposema hatuwezi tukasahau, tunamaanisha vivyo hivyo''.
Ziara hiyo inakuja siku moja baada ya rais wa Marekani kusema hatachapisha picha ya mwili wa Osama Bin Laden.
Kiongozi huyo wa Al-Qaeda aliuwawa na vikosi maalum vya jeshi la Marekani kaskazini mwa Pakistan siku ya Jumatatu.
Baadaye mwili wake ulizikwa kwenye bahari kutoka kwa ndege ya Marekani iliyokuwa imembeba.
Majeshi ya Pakistan yalikiri kushindwa kugundua alikojificha Bin Laden na kusema wataanzisha uchunguzi.
Pakistan pia imedokeza kuwa itatizama upya ushirikiano kati yake na Marekani iwapo kutatokea uvamizi mwingine bila ya wao kufahamishwa kama ilivyofanyika na Osama bin Laden.

Mji wa Homs walengwa na vifaru

Watu wasiopungua 1000 waliimba nyimbo za kuunga mkono wenzao wa mji wa Deraa ulio kusini mwa nchi ambako vikosi vimekuwa vikiwakamata mamiya ya wanaume katika misako ya nyumba hadi nyumba.
 Rais Assad achukiwa
picha yachomwa
Kote nchini Syria watu 2,843 inaaminika wamekamtwa na kufungwa. Wanaharakati wanasema kuwa idadi kamili huenda ni watu 8000 ambao wamekabiliwa na mateso kutoka majeshi.
''Marekani yasema hatua ya Syria ni unyama''
Makundi ya kutetea haki yamesema kuwa takriban watu 560 wameuawa kote nchini katika maandamano dhidi ya utawala dhalimu wa Rais Bashar al-Assad.
Maandamano yaliyoanza tarehe 15 mwezi Machi, ndiyo tishio kubwa kuwahi kutokea katika miaka arobaini ya utawala wa familia ya Assad katika mojapo ya nchi zenye sera ya kuwabana wananchi kwa sheria kali kupindukia.

Ouattara wa Ivory Coast aapishwa

Alassane Ouattara anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa Ivory Coast na mtu ambaye mwanzo alimkatalia ushindi wake katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Novemba.
Mwezi Desemba, kiongozi wa baraza la katiba alimwidhinisha Laurent Gbagbo kuwa mshindi, iliyosababisha nafasi hiyo kushikiliwa naye kwa muda wa miezi minne.
Bw Gbagbo pia anatarajiwa kuhojiwa juu ya madai ya kukiuka haki za binadamu wakati akiwa madarakani.
Bw Alassane Ouattara
Hata hivyo, imeripotiwa kuwa mawakili wake kutoka Ufaransa wamenyimwa ruhusa ya kuingia Ivory Coast.
Shirika la habari la AFP limesema walizuiwa kwenye uwanja wa ndege wa Abidjan na kutiwa kwenye ndege iliyofuata na kurejeshwa Paris.
Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya unatarajiwa kuipa nchi hiyo msaada wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 60.
Kamishna wa maendeleo wa Ulaya, Andris Piebalgs, ambaye yupo Ivory Coast, amesema inabidi waende kwa kasi.
Aliiambia BBC kuwa hali ilivyo nchini humo bado ina utata na kama maisha ya watu hayakuimarishwa haraka, ghasia zinaweza kuanza upya.
Alisema raia wa nchi hiyo wanahisi wamepoteza miaka 25 ya maendeleo kutokana na mapigano ya kisiasa na kikabila ya hivi karibuni.
Takriban watu 3,000 wanaaminiwa kuuawa wakati wa ghasia zilizotokea kwenye nchi inayozalisha kakao zaidi duniani, ambapo awali ilikuwa nchi yenye utajiri mkubwa Afrika magharibi.