Saturday 28 July 2012

Kaburu anahatia kupanga kumuua Mandela


Mike du Toit ana hatia ya kutaka kumuua Mandela
Mtu aliyepanga njama za kutaka kumuuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amepatikana na hatia.
Mahakama ya Pretoria ilimpata kiongozi wa kundi la -Boeremag linaloamini kuwa mtu mweupe ni bora alipatikana na hatia ya kupanga kummua Mandela mwaka 2002.
Bwana Mike du Toit ndiye aliyepanga milipuko tisa katika eneo la Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.
Kiongozi huyo wa kundi la ki-baguzi ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia tangu utawala wa wengi uanze mwaka 1994 Afrika kusini.
Wachanganuzi wanasema kuwa bado kuna hali ya kutopendana katiki ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini.
Hata hivyo kundi kama la Boeremag,inayomaanisha Nguvu za Makaburu miongoni mwa Makaburu ,halina ufuasi mkubwa.
Mahakama hiyo ya Pretoria imempata Du Toit, ambaye alikuwa msomi baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa miaka tisa.

London 2012, sherehe za ufunguzi zanukia


Shamra shamra za London
Familia ya kifalme imeukaribisha Familia ya kifalme imeukaribisha mwenge wa Olimpiki katika Kasri la Buckingham katika siku ambapo umati mkubwa wa watu ulikusanyika mjini London kushuhudia mkondo wa mwisho wa safari ya mwenge huo mjini London.

Mwenge huo kadhalika uliwasilishwa Downing Street, makao makuu ya serikali ya Uingereza.
Baada ya tetesi kuzuka kuhusiana na maandalizi ya michezo hiyo, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema michezo ya mwaka huu itathibitisha kuwa Uingereza ina uwezo wa kufanya maandalizi kabambe.
Lenye Ijumaa ndiyo siku ya ufunguzi rasmi wa mashindano yatakayopeperushwa moja kwa moja kote duniani.

Bwana Cameron ametetea maandalizi ya mashindano hayo baada ya mgombea wa kiti cha urais nchini Marekani Mitt Romney kusema kwenye mahojiano katika runinga ya NBC kwamba kuna matatizo katika usalama na tishio la mgomo wa maafisa katika maeneo ya mipakani.
Lakini baadaye bwana Romney alitabiri kuwa mashindano ya Olimpiki mjini London yatakuwa yenye mafanikio baada ya kukutana na waziri mkuu huko Downing Street.
Hapa Bw. Cameron aliukaribisha mwenge huo wakati uliposimama kwa muda ukiwa njia kuelekea Kasri la Buckingham.
Mwanamfalme William, mkewe na mwanamfalme Harry walikuwepo kuwakaribisha waliokuwa wakiiperusha mwenge huo kabla ya kupelekwa Hyde Park.
Meya wa mji wa London Boris Jonnson akizungumza mbele ya umati mkubwa wa watu 60,000 waliojitokeza kushuhudia sherehe hiyo aliwatakiwa kila la heri na kusema ''mashindano ya London yatakuwa ni ya kukata na shoka.''
Lakini pia alizungumzi mzozo uliokuwepo awali aliposema mbele ya umati huo: "kuna mtu anayeitwa Mitt Romney ambaye anataka kujua ikiwa tuko tayari. Tuko tayari? Ndiyo tuko Tayari!"

Michezo ya Olimpiki yaanza hasa.

Shereh za ufunguzi wa mIchezo ya Olimpiki mjini London

Mashindano mbali mbali yaanza hasa Jumamosi katika michezo ya Olimpiki mjini London.
Moja ya michezo hiyo ni mashindano ya mbio za wanaume za baiskeli, lakini piya kuna gymnastics, kuogelea na basketboli.
Watu zaidi ya 15,000 walijitolea na kushiriki kwenye tamasha ya ufunguzi wa michezo Ijumaa usiku -
tamasha la fakhari la mchanganyiko wa watu, tamthilia na muziki.
Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa, Jacques Rogge, alisema sherehe hiyo ya ufunguzi ilionesha yote yaliyo mazuri katika ubunifu wa Uingereza.