Wednesday 4 May 2011

BOB JUNIOR: SITAMSAMEHE WEMA

Na Brighton Masalu
PRESIDENT wa Masharobaro, Raheem Nanji Rummy ‘Bob Junior’ amefunguka na kusema kwamba, kamwe hawezi kumsamhe mlimbwende wa 2006, Wema Isaac Abraham Sepetu kwa kitendo chake cha kumtukana japo mrembo huyo ameonesha dalili za kumuomba msamaha kupitia kwa wazazi.

Akizungumza na ‘Vuvuzela’ wa gazeti hili ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Bob Junior alisema kuwa si rahisi yeye kukubali msamaha kwani Wema ameingilia ugomvi ambao haukuwa wake na kumtukana matusi yaliyomdharirisha, hivyo ni lazima sheria ifuate mkondo wake.
“Mimi siwezi kumsamehe Wema hata siku moja, kwani kitendo chake cha kunitukana hakikunifurahisha, maana yeye hajui kuwa chanzo cha bifu lilipo baina yangu na msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambaye ni bwana yake, linatokana na wivu wa kimaendeleo ambao Diamond unamsumbua,” alisema Bob Junior na kuongeza:

“Tena sihitaji hata fedha ya aina yoyote kutoka kwake, ilimradi tayari kesi inaendelea, hivyo nimeacha sheria ichukue mkondo wake. Nataka nimfundishe kwa njia ya sheria japokuwa tayari ameshaanza kuniomba msamaha kupitia watu wengine wakiwemo wazazi,” alimaliza Bob Junior.
Hivi karibuni Bob Junior alimfungulia mashitaka mrembo huyo kwa kitendo chake cha kumtukana kwa njia ya simu.

No comments: