Friday, 6 May 2011

Watoto wa aliyekuwa Mfalme wa Mziki wa Pop Michael Jackson watoa msaada kwa waathirika wa Sunami Japan

WATOTO wa aliyekuwa mfalme wa pop, Michael Jackson, wameguswa na janga lililoikumba Japan hivi karibuni na kuamua kuchangia nguo za kuwapa walioponyeka kwenye maafa hayo.
Shangazi wa watoto hao, La Toya Jackson, alibainisha watoto hao, Prince Michael, Paris na Blanket wameguswa moja kwa moja na tukio hilo na hivyo kuamua kutoa walichonacho kwa watoto wenzao.
Michango mbalimbali ya misaada imekuwa ikihamasishwa kutolewa kwa ajili ya kuwasaidia walioathirika na janga la tetemeko la tsunami na watoto hao wa nyota wa muziki wa pop duniani, Michael Jackson wamebainisha kuwa na kitu kidogo cha kuchangia.


La Toya aliiambia OKmagazine.com, “Hawakujali wanafanya nini au wanatoa kitu gani. Ilikuwa safi sana. Walisema, ‘Tunaweza kuwapa nguo zetu?’ Ilikuwa safi sana.”
La Toya alisema kwamba familia ya Jackson imefarijika kwa kuwapeleka watoto hao wa mwimbaji wa “Thriller” katika matukio kama hayo ya michango ya kihisani.

No comments: