PRESIDENT wa Masharobaro, Raheem Nanji Rummy ‘Bob Junior’ amefunguka na kusema kwamba, kamwe hawezi kumsamhe mlimbwende wa 2006, Wema Isaac Abraham Sepetu kwa kitendo chake cha kumtukana japo mrembo huyo ameonesha dalili za kumuomba msamaha kupitia kwa wazazi.
Akizungumza na ‘Vuvuzela’ wa gazeti hili ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni Jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Bob Junior alisema kuwa si rahisi yeye kukubali msamaha kwani Wema ameingilia ugomvi ambao haukuwa wake na kumtukana matusi yaliyomdharirisha, hivyo ni lazima sheria ifuate mkondo wake.
“Tena sihitaji hata fedha ya aina yoyote kutoka kwake, ilimradi tayari kesi inaendelea, hivyo nimeacha sheria ichukue mkondo wake. Nataka nimfundishe kwa njia ya sheria japokuwa tayari ameshaanza kuniomba msamaha kupitia watu wengine wakiwemo wazazi,” alimaliza Bob Junior.

No comments:
Post a Comment