STAA kunako tasnia ya filamu Bongo,Flora Festo Mvungi (pichani) ameibuka na kujibu kauli iliyotolewa na mama yake mzazi, Zuhura Mvungi kuwa hamtambui mchumba wake ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva, Hamis Ramadhani Baba ‘H-Baba’, mistari hapa chini ina mkanda mzima.
Akizungumza na gazeti hili ndani ya New Maisha Club, Masaki jijini Dar es Salaam, msanii huyo alitambaa na vina kuwa, alishtushwa sana na kauli ya mama yake kutomtambua mchumba wake, jambo ambalo halina ukweli hata kidogo na kudai kuwa alishawahi kuonana naye mara kwa mara na kama haitoshi huwa anawasiliana naye kwa njia ya simu.
“Aisee nilipatwa na mfadhaiko mkubwa sana juu ya kauli ya mama na sikuamini kama mama yangu mzazi anaweza kutamka maneno kama yale, kwani anafahamiana vizuri sana na H-Baba na walishakutana na bado huwa wanawasiliana kwa simu,” alisema Mvungi na kuongeza:
“Nikimaliza kazi niliyonayo kwa sasa, nitakuchukua hadi nyumbani uongee na mama nami nikiwepo, tuone atajibu nini yaani mama simuelewi kabisa lakini kwa kuwa yeye ni mzazi labda aliamua kusema hivyo akiwa na lengo lake lakini ninachojua ni kwamba mama anafahamiana vizuri sana na mchumba wangu huyo,” alimaliza msanii huyo.
“Aaah, mimi bwana sitaki tena kuongelea sana habari hizo maana yamesemwa mengi sana juu yangu, aliyoyasema Flora yanatosha na pengine mama alisema hayo kwa maana yake na siwezi kumchukia hata kidogo,” alifunga taya msanii huyo.
Awali, paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakiwa wamekaa kwa staili ya kumbikumbi mbele ya kaunta ukumbini hapo huku wakipata vinywaji.
Hivi karibuni mama mzazi wa Flora alitoa kauli iliyowaacha watu wengi midomo wazi, baada ya kutamka kuwa hamtambui hata kidogo mchumba wa mwanaye ambaye ni H-Baba.
No comments:
Post a Comment