Tuesday, 3 May 2011

Mke na doezi huyo walipotoka nje

Na Shakoor Jongo
FUMANIZI lililotokea alfajiri ya kuamkia Aprili 25, mwaka huu limezua ajali baada ya jamaa aliyedaiwa kutembea na mke wa rafiki yake kutoroka na mwanamke huyo na gari walilopanda kuligonga daladala linalofanya safari zake kati ya Ubungo na Msasani jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilianzia ndani ya New Maisha Club, Msasani jijini Dar wakati wagoni hao walipokuwa wakila raha na kabla ya mwenye mali kutokea na kuwafanya watimue mbio.

kwa mujibu wa paparazi wetu aliyeshudia kisanga hicho, jamaa alipomuona rafiki yake  mwenye mke akiingia ndani ya klabu hiyo, aliamua kutimua mbio kupitia  mlango mwingine kutoka nje ya ukumbi huo akiwa sambamba na mwanmke huyo.

Mke na doezi huyo walipotoka nje, waliingia ndani ya gari na kutimua mbio kwa fujo hali iliyowashtua watu wengi.

Kwa kuwa mume alishawaona naye akawakimbiza hadi nje ya ukumbi huo na alipofika nje akadandia Bajaj na kumwamuru dereva kuifukuza gari ile, paparazi wetu naye akadandia gari nyingine kwa ajili ya kufuatilia mchezo mzima.

Safari ya wagoni hao iliishia kwenye mataa ya Morocco, Kinondoni baada ya mwanaume huyo kukumbwa na mcheche kwa kujua gari la mwandishi wetu ndilo alilokuwa akija nalo rafiki yake ambaye ndiye mwenye mke.
Hivyo, mwanaume huyo alishindwa kuhimili kona ya kuelekea Mkwajuni na kwenda kulivamia daladala na kusababisha ajali mbaya.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, shuhuda ambaye anawajua watu hao kiundani zaidi alisema kuwa, anawafahamu wahusika waliopata ajali kama mtu na shemeji yake na walikuwa wakitoka pamoja na mume wa mwanamke huyo siku za nyuma.

“Mume wa mwanamke namjua na huyu jamaa ni shemeji yake, siku zote wamekuwa wakitoka watatu pamoja na  mume mtu nashangaa leo kuwaona  wakiwa wawili,” kilisema chanzo hicho.

Naye, mlinzi wa Maisha Club ambaye (jina lake linawekwa kapuni) aliyekuwepo katika msafara wa kulikimbiza gari la wagoni hao, alisema kuwa tukio hilo limewachanganya kwa kuwa hawakuwa wakijua kama jamaa alikuwa akimchukua mke wa rafiki yake.

Baada ya kusikiliza upande mmoja wa habari, paparazi wetu aliamua kumhoji jamaa aliyekuwa akitoroka na mke wa rafiki yake, hata hivyo aligoma kuzungumza kisha kupotea  katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la tukio.

Mpaka watu wanatawanyika katika tukio hilo la ajali, mume aliyekuwa akiwakimbiza wagoni wake kwa kutumia kibajaji hakujulikana alipoishia.

No comments: