Chakula kimepungua maeneo ya waasi
Waasi wa Libya wametoa mwelekeo wa kisiasa kwa nchi hiyo iwapo Kanali Gaddafi ataondoka madarakani.
Mwelekeo huo unaonyesha kuanzishwa kwa serikali ya mpito wakati katiba mpya inaandikwa na uchaguzi kufanyika.
Mahmoud Jibril alitoa pendekezo la Libya baada ya Kanali Gaddafi katika mkutano wa kwa wajumbe wa nchi zinazounga mkono waasi uliofanyika Rome Italia.
Alifafanua kuwa serikali ya mpito itaanza kazi mara moja ili kutoa maekezo ya utendaji wa siku kwa siku na kuweka ulinzi, shirika la habari la AFP imeripoti.
Mahmoud Jibril,kiongozi wa Baraza la Kitaifa la Mpito (NTC) amekubaliana na mpango wa misaada uliopitishwa na nchi 22 zinazounga mkono waasi hao.
Katika habari nyingine, Ufaransa imewaamuru wanadiplomasia 14 wa Libya wanaomuunga mkono Kanali Gaddafi kuondoka nchini humo ndani ya siku mbili.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa alisema maafisa hao wametajwa kuwa 'watu wasiotakiwa nchini humo.'
No comments:
Post a Comment