Tuesday, 10 May 2011

Rais wa zamani Niger kuachiliwa

Bw Mamadou Tandja
Mahakama ya Rufaa nchini Niger imeamuru kuachiliwa mara moja kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Mamadou Tandja aliyepinduliwa mwezi Februari 2010.
Tangu wakati huo Bwana Tandja alikuwa madarakani kwa miaka 10, anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.
Viongozi wa mapinduzi hayo walikasirishwa baada ya Tandja kuwania uongozi tena kwa kipindi kingine cha tatu.
Mwezi uliopita, uongozi huo wa kijeshi ulikabidhi rasmi utawala kwa kiongozi wa upinzani wa siku nyingi Mahamadou Issoufou aliyeshinda uchaguzi wa marudio mwezi Machi.
Katika mzunguko wa kwanza mwezi Januari Tandja aliondolewa kutoka kwenye nyumba aliyowekwa kizuizini na kupelekwa gerezani.
"Mashtaka yote na kesi dhidi ya Mamadou Tandja yamefutwa" mmoja wa wanasheria wake Souley Oumarou, ameliambia shirika la Habari la AFP.
Mwandishi wa BBC nchini Niger Idy Baraou anasema Tandja alikuwa anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za serikali kiasi cha dola milioni moja.
Alikuwa pia anahusishwa na ufisadi wa zabuni ya mbolea yenye gharama kati ya $9m na $10m.
Katiba mpya ya Niger imepunguza madaraka ya Marais wanaokuja na kuweka kikomo cha urais kuwa miaka kumi.

No comments: