Friday, 6 May 2011

Fainali ya wanavitimbi,Je ni nani atajinyakulia ushindi kati ya hawa?

Lile shindano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa vichekesho Bongo, linatarajiwa kufanyika kesho ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, Dar es Salaam ambapo patakuwa hapatoshi.

Akizungumza na Ijumaa, mratibu wa shindano hilo, Imelda Mtema alisema kuwa,  mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan na kiingilio kitakuwa shilingi 8,000.

Aidha, mratibu huyo alisema kuwa, washiriki wote wa shindano hilo lililoendeshwa na Gazeti la Risasi kwa muda wa miezi minne, wamejiandaa vizuri.

Alizitaja zawadi za washindi kuwa, mshindi wa kwanza ataondoka na kitita cha Tsh.1,500,000, wa pili 1,000,000 na 500,000 kwa mshindi wa tatu.

Washiriki watakaoshika nafasi ya nne na tano, watapata kifuta jasho cha Tsh. 250,000.
Shindano hilo litapambwa na burudani kutoka Bendi ya muziki wa dansi nchini,  African Stars International ’Twanga Pepeta’ na wasanii wa miondoko ya kizazi kipya, Sam Morgan, TMK Unit, Tox Star na Ziro 4.

Shindano hilo limedhaminiwa na Allure International Model, Dar es Salaam City College- Kimara, Jarida la Malaika, Cream Pub- Kinondoni, Dotnata Decoration, Manywele Beauty Cosmetics na ASET Ltd.

Washiriki waliotajwa kuwania tuzo hizo ni Joti, King Majuto, Masanja Mkandamizaji, Kingwendu (pichani) na Masele.

Kama unawafagilia, endelea kupiga kura, unaweza ukamsaidia yule unayetaka aibuke mshindi.
Jinsi ya kupiga kura, andika jina la mshiriki unayependa ashinde katika sehemu ya ujumbe wa simu kisha tuma kwenda 0788 240 136

No comments: